You are currently viewing Ommy Dimpoz aachia rasmi album yake mpya

Ommy Dimpoz aachia rasmi album yake mpya

Mwimbaji nyota wa muziki nchini Tanzania, Ommy Dimpoz ameachia rasmi album yake mpya iitwayo Dedication kupitia majukwaa mbalimbali ya ku-stream muziki mitandaoni.

Album hiyo yenye jumla ya ngoma 15, imewakutanisha wanamuziki wengine kama Marioo na Nandy toka Tanzania, na nje ya Tanzania ni Blaq Diamond, Fally Ipupa, The Ben, DJ Maphorisa, DJ Kerozen, Kabza na Julio Masidi.

Mtayarishaji mkuu wa album hiyo ni ommydimpoz mwenyewe ikiwa pia ndio album yake ya kwanza kuiachia katika safari yake ya muziki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke