You are currently viewing OMMY DIMPOZ AFUNGUKA SABABU YA KUTOWEKA WAZI MAHUSIANO YAKE YA KIMAPENZI

OMMY DIMPOZ AFUNGUKA SABABU YA KUTOWEKA WAZI MAHUSIANO YAKE YA KIMAPENZI

Msanii wa Bongofleva, Ommy Dimpoz amesema kuwa wasichana wengi wanatamani kuolewa na yeye na kila mara amekuwa akipokea maombi yao.

Ommy Dimpoz amesema hayo kwenye Podcast ya Lil Ommy ambapo ametaja hiyo ni moja ya sababu ya kutomuweka wazi mpenzi wake rasmi kwani anajua kufanya hivyo atawaumiza wengi.

“Kuna wasichana wengi sana kila siku wanalia nioe mimi, hizo nishazoea, ni kawaida, nina uhakika na watu wengine inawatokea lakini mimi naweza kuwa baba yao kwenye suala hilo” amesema Ommy.

“Lakini katika suala hilo (kuoa) mimi Muislamu naruhusiwa hao wanne, kwa hiyo inawezekana hata sasa hivi nina hao wanne wa kuwapima, kwa hiyo time itakapofika haina shida,” amesema.

Ommy Dimpoz anayefanya vizuri kwa sasa na wimbo wake mpya, Umeniweza, ameongeza kuwa kwa sasa hana mtoto lakini kabla ya mwaka huu kuisha mambo yanaweza kuwa mazuri, yaani kupata mtoto.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke