You are currently viewing OMMY DIMPOZ AKIRI KUWAHI KUWEKEA SUMU ILI AFE

OMMY DIMPOZ AKIRI KUWAHI KUWEKEA SUMU ILI AFE

Nyota wa muziki nchini Tanzania, msanii Ommy Dimpoz amekiri mbele ya mashabiki kuwahi kuwekewa sumu ili afe, katika tukio lilitokea mwaka 2018 lililomfanya akafanyiwa oparesheni tatu kubwa ya koo lake akipambania kuokoa maisha yake.

Akiwa na mwimbaji Christian Bella, ndani ya ‘Break Point’ Makumbusho, waliitumbiza pamoja kolabo yao “Nani Kama Mama” ambapo kwenye verse yake Ommy Dimpoz alisikika akisema, “Sumu Waliniwekea, Bado Nusu Nikufuate Mama” akiwa na maana kwa sasa angekuwa marehemu, kwani ilibaki kidogo amfuate mama yake ambaye ameshatangulia mbele za haki.

Ommy Dimpoz ambaye ameuanza vyema mwaka huu akiwa tayari ameachia ngoma mbili, aliwahi kusema athari ya koo lake ni matokeo ya sumu. Na kwenye interview yake na Millard, Ommy alisimulia sauti yake ilivyorudi, ni kabla hajapelekwa Ujerumani alikofanyiwa oparesheni ya tatu ambayo ilikuwa ya mwisho.

Ikumbukwe, ni takribani miaka mitatu sasa imepita Dimpoz hakuonekana jukwaani akitumbuiza.

Hata hivyo hii inakuwa mara yake ya pili baada ya Machi 20 mwaka huu, kutumbuiza kwenye tamasha lake aliloliita “Cheusi Cheupe” lililofanyika katika viwanja vya Zakhem, Mbagala jijini Dar es salaam.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke