Mwanamuziki Ommy Dimpoz ametangaza rasmi jina la Album yake mpya na ya kwanza kwenye Muziki, inaitwa ‘Dedication’ na itakuwa na Jumla ya nyimbo 15.
Album hiyo ambayo itaachiwa November 4 mwaka huu, Dimpoz amewapa shavu wakali wa Afrika akiwemo Nandy, Fally Ipupa, Blaq Diamond, The Ben na wengine.
Aidha, kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameeleza kwamba haikuwa rahisi kuikamilisha album hiyo ukizingatia mapito aliyoyapitia miaka ya hivi karibuni.
Hata hivyo ametoa shukrani zake za dhati kwa wote waliomsaidia kufika alipo leo ikiwemo familia yake pia.