You are currently viewing OMMY DIMPOZ KWA MARA YA KWANZA AFUNGUKA CHANZO CHA UTAJIRI WAKE

OMMY DIMPOZ KWA MARA YA KWANZA AFUNGUKA CHANZO CHA UTAJIRI WAKE

Msanii wa Bongofleva, Ommy Dimpoz amefunguka wapi anapopata fedha ambazo ameonekana akila nazo bata sehemu mbalimbali duniani na kuendesha magari ya kifahari.

Katika mahojiano na Podcast ya Swahili Nation, Dimpoz amesema kitu kimoja katika maisha unachotakiwa kujua ni kujiongeza mara baada ya kutengeneza jina ambalo ndilo msingi wa kupata dili.

“Kujiongeza ni kitu kimoja muhimu sana kwa sababu umeshatengeneza jina, jina lako linakusaidia vipi, unatengeneza vipi michongo na sio kila kitu it’s about money,” amesema.

Ameendelea kwa kusema, “Mimi ni balozi wa GSM toka 2016, sitaki kukuambia nalipwa shilingi ngapi lakini nalipwa kila mwezi, lakini pia mimi ni creative director, matangazo yote unayoyaona ya GSM na kuisimamia mitandao yao ya kijamii ni kazi yangu mimi kupitia kampuni yangu lakini sina haja ya kuja kuwaambia watu”.

Hitmake huyo wa ngoma ya “Hello Baby” amefunguka kuhusu kuwa kwenye bifu na Ali Kiba kwa kusema kuwa kama kungekuwa na ugomvi kati yake na Ali kiba kama inavyo inadaiwa, ingeonekana wazi ila kwa sasa bado wao ni kama familia.

“Alikiba bado ataendelea kuwa kaka yangu kwenye muziki hata kifamilia, yaani yeye nishampa nafasi kwamba huyu ni Kaka amechukua nafasi kubwa kwenye maisha yangu ukiachana na mambo ya muziki. Hata ikitokea leo tumekwaruzana maana sisi ni binadamu lakini nina nafasi kubwa ya kusamehe na kusonga mbele,” amesema.

“Hakuna mahali tumegombana, wimbo huu, Umeniweza unaona ame-share kwenye page yake, sasa wewe anamjua Alikiba kama hataki, hataki, na humbadilishi, hajuai kuigiza. Kwa hiyo kungekuwa na tatizo, mngejua na kwenye uzinduzi wa albamu yake nisingekuwepo, na mimi siwezi kwenda sehemu ambayo sijaalikwa”, amesema Ommy Dimpoz.

Utakumbuka Ali kiba na Ommy Dimpoz ambao wamewahi kufanya ngoma tatu pamoja, kuna wakati walikuwa chini ya usimamizi wa Rockstar Africa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke