Album mpya ya msanii Ali kiba “Only One King” inazidi kuweka historia mara baada ya cover la album hiyo kuonekana katika Screen za eneo maarufu Times Square huko Jijini New York, nchini Marekani.
Album hiyo ambayo ina siku tatu tangu iachiwe, ina kuwa kazi ya kwanza Kwa Ali kiba kuonekana Times Square sehemu ambayo matangazo makubwa duniani huonekana.
Sanjari na hilo “Only One King” album imefanikiwa kufikisha jumla ya Streams Milioni 1 katika mtandao wa BoomPlay tangu iachiwe rasmi Oktoba 7.
Album hiyo ambaye ni ya tatu kwa mtu mzima Ali Kiba ina nyimbo 16 alizoshirikisha wasanii kutoka Tanzania, Kenya na Nigeria.
Miongoni mwa nyimbo zilizoko ni Utu, Let me, Niteke, Bwana mdogo, Happy, na nyingine nyingi.