You are currently viewing OS SSUNA AFUNGUKA SABABU ZA KUBADILI DINI

OS SSUNA AFUNGUKA SABABU ZA KUBADILI DINI

Bosi wa lebo ya muziki ya White House Music Entertainment  Emmanuel Suna maarufu kama Os Suna amefunguka sababu za kubadilisha dini kutoka ukristo kwenda uislam.

Akiwa kwenye moja ya interview Suna amesema alipata wito wa kubadili dini kutoka kwa mwenyezi mungu na hakuna jinsi hangezuia jambo hilo kufanyika.

Hitmaker huyo wa Siri Gambler amekanusha madai yanayotembea kwenye mitandao ya kijamii kuwa alibadili dini na kuwa muislamu kwa sababu alilazimishwa na mwanamke aliyetaka kumuoa kipindi hicho.

Suna amesema wakati aliacha dini ya ukristo alirudi kwa wana familia wake na kuwaomba msamaha kwa hatua ya kubadili dini bila ya kuwataarifu.

Hata hivyo amejinadi kwa kusema kwamba kipindi anakumbatia dini ya kiislam alikuwa na mafanikio makubwa kimuziki kwani nyimbo zake zilifanya vizuri kwenye chati mbali mbali nchini uganda.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke