You are currently viewing OTIILE BROWN AFUNGUKA KUHUSU MAISHA YAKE YA MAHUSIANO

OTIILE BROWN AFUNGUKA KUHUSU MAISHA YAKE YA MAHUSIANO

Nyota wa muziki nchini Otile Brown, amesema licha ya kusumbuliwa na warembo kwa sasa hayupo kwenye mahusiano,yaani yupo ‘Single’.

Mkali huyo anayefanya vizuri na EP yake mpya Uptown Flex amedai kwa sasa hataki kukurupuka kuingia kwenye mahusiano ya mapenzi kutokana na matukio aliyopitia kipindi cha nyuma.

Otile Brown amefunguka hayo  kwenye Instagram live, mara baada ya mashabiki zake kutaka kujua upande wa maisha yake ya mahusiano baada ya kutangaza kuachana na mrembo mwenye asili ya nchi ya Ethiopia Nabayet wiki kadhaa zilizopita.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke