Mwanamuziki kutoka Kenya Otile brown ameachia rasmi Extended playlist yake mpya baada ya ukimya wa miezi mitatu
EP hiyo iitwayo Terminator ina jumla ya nyimbo tano za moto akiwa amewashirikisha wakali kama Vivian, Ilogos na The Ben.
Terminator EP ina nyimbo kama Kolo Kolo, Terminator, By My Side, Hatima, Do It na inapatikana Exclusive kwenye majukwaa yote ya kupakua na kusikiliza muziki mtandaoni.
Hii ni EP ya pili kwa mtu mzima Otile Brown baada ya Uptown Flex iliyotoka mapema mwaka huu ikiwa na jumla ya singles 4 za moto.