You are currently viewing OTILE BROWN ADAI MBOSSO NA ZUCHU WAMEIBA MELODY YA WIMBO WAKE

OTILE BROWN ADAI MBOSSO NA ZUCHU WAMEIBA MELODY YA WIMBO WAKE

Nyota wa muziki Otile Brown ameingia kwenye headline katika mitandao ya kijamii  mara baada ya kudai kuwa Mbosso ameiiba idea ya wimbo wake na kuitumia kwenye wimbo wake mpya uitwao”For You Love” ambao amemshirikisha Zuchu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Otile Brown amedai kwamba Mbosso na Zuchu waliiba mdundo wa wimbo wake uitwao “Baby Love” na kuutumia kwenye wimbo wao bila ridhaa yake.

Hitmaker huyo wa “Jeraha” amedai kwamba angekuwa na roho mbaya angeweza kuiripoti ngoma hiyo kwa Youtube kama njia ya kudai hakimiliki.

Suala hilo limeibua maswali mengi miongoni mwa wadau wa muziki nchini ambao wameenda mbali zaidi na kuhoji kuwa Otile Brown  anataka kutumia jina la Mbosso na Zuchu kujitafutia umaarufu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke