Staa wa muziki nchini Otile Brown amewajibu wanaodai kuwa anajipendekeza kwa mpenzi wake wa zamani Nabayet licha ya mahusiano yao kuvunjika.
Otile ambaye amerejea nchini baada ya kukamilisha ziara ya miezi miwili nchini marekani amewashangaa wanaomsema vibaya kuwa bado anamzimia kimapenzi mrembo huyo kwa kusema kuwa hajutii kitendo cha kumtumia salamu za heri kwenye kumbukizi ya kuzaliwa kwake kwani ni moja kati ya watu ambao anawapenda sana.
Otile Brown na Nabayet walikuwa kwenye mahusiano kwa kipindi cha miaka miwili lakini mahusiano yalikuja kuvunjika mwaka wa 2020 kutokana na umbali kati yao.
Utakumbuka mwaka wa 2019 Otile Brown aliachia wimbo wa kusifia urembo wa Nabayet baada ya penzi lao kunoga.