You are currently viewing OTILE BROWN AFUNGUKA NAMNA WANIGERIA WANATEGEMEA SOKO LA KENYA KUTANGAZA MUZIKI WAO

OTILE BROWN AFUNGUKA NAMNA WANIGERIA WANATEGEMEA SOKO LA KENYA KUTANGAZA MUZIKI WAO

Staa wa muziki nchini Otile Brown Otile Brown amefunguka jinsi ambavyo Wanigeria wanatumia soko la muziki wa Kenya kutangaza muziki wao

Kulingana na Otile Brown wasanii wa Nigeria wanategemea soko la Kenya kufanya nyimbo zao ziwe kubwa zaidi kwa kuwa wanatumia pesa nyingi kuhonga vituo vya redio nchini ili viweze kucheza nyimbo zao.

Hitmaker huyo ngoma ya “Woman” amesema nyimbo nyingi za Nigeria zimeshindwa kupenya kwenye soko la muziki hadi pale wakenya kwenye mtandao wa tiktok wanapoanza kuzitumia kwenye video zao.

Hata hivyo ametoa changamoto kwa vyombo vya habari  nchini kuunga mkono kazi za wasanii wa humu nchini bila kubagua ili muziki wa kenya uweze kutabulika katika mataifa mengine.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke