Siku chache tu baada ya kufanyiwa upasuaji, mwanamuziki kutoka Kenya, Otile Brown amewaacha mashabiki wake katika hali ya wasiwasi kutokana na chapisho lake kwenye mitandao ya kijamii.
Otile Brown ametoa taarifa fupi kuhusu afya yake akifichua kwamba anashuhudia maumivu makali sana mwili mwake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram amewasihi mashabiki wake kumkumbuka katika maombi yao huku akiendelea kuuguza maumivu yanayomkabili.
“Nina maumivu makali sana, ombeeni Obizee” Brown ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Utakumbuka takriban siku tano zilizopita mwanamuziki huyo alifanyiwa upasuaji katika hospitali moja jijini Nairobi. Hata hivyo,hakueleza sehemu ya mwili wake ambayo ilifanyiwa upasuaji wala kilichokuwa kinamsumbua.