Nyota wa muziki nchini Otile Brown amefunguka kuhusu sakata la msanii wa Nigeria Fave kudhulumiwa na promota baada ya kukamilisha ziara yake ya kimuziki nchini.
Kupitia instastory Otile amesema pana haja ya mapromota wa Kenya kuchukulia biashara kama suala la muda mrefu badala ya kuwadhulumu washirika wao ambao wana mchango mkubwa kwenye mafanikio ya shughuli zao.
Hitmaker huyo wa “Celebration” amewakosoa mapromota waliomleta Fave nchini Kenya kwa kutokuwa na mipango mizuri ya kufanikisha show ya msanii huyo huku akisisitiza kuwa mawasiliano ni jambo la msingi kwenye biashara yeyote yenye mafanikio.