Staa wa muziki nchini Otile Brown ameonesha kukerwa na kitendo cha Arrow Boy kuushirikisha wimbo wao wa pamoja ambao haukuwa umekamilika kwenye album yake mpya iitwayo Focus.
Kupitia instastory Otile Brown ametaja Arrow Boy kama mnafiki asiyejali maslahi ya wasanii wenzake kwa hatua yake ya kukwenda kinyume na mkataba wa makubaliano wa kutoachia demo ya wimbo wao wa pamoja huku akisema kwamba kitendo hicho huenda ikamshushia brand yake ya muziki.
Hata hivyo wa ngoma ya “Fine By Me” amemtaka Arrow Boy auondowe wimbo wao uitwao “Show Me” kwenye album yake ya Focus kabla hajachukua hatua ya kuishusha mwenyewe wimbo huo kwenye digital platforms mbali mbali za kupakua na kusikiliza muziki duniani.