Staa wa Muziki Nchini Otile Brown ameshindwa kujizuia na kufunguka hadharani jinsi anavyomukubali Msanii wa Kike kutoka Tanzania Abby Chams.
Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Otile ameonesha kuukubali uwezo wa Mrembo huyo kwa kushare picha ya wimbo wa Rayvanny aliomshirikisha Abby Chams, STAY na kuandika ujumbe unaosomeka ” abby_chams Mashallah coming to tanzania anytime Inshallah hopn to meet you queen ”
Ujumbe huo umewaaminisha mashabiki kuwa huenda wawili wana mpango wa kuja na wimbo wa pamoja hivi karibuni.
Iwapo Otile Brown atafanikisha suala la kuachia wimbo wa pamoja na Abby Chams itakuwa ni kazi yake ya tatu kufanya na msanii wa Bongofleva ikizingatiwa tayari ana collabo na Ali Kiba na Harmonize.