You are currently viewing OTILE BROWN AKOSHWA NA MFUMO WA MUZIKI WA AFRIKA KUSINI

OTILE BROWN AKOSHWA NA MFUMO WA MUZIKI WA AFRIKA KUSINI

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya Otile Brown ameusifia mfumo wa muziki wa Afrika Kusini ambao ameutaja kuulinda zaidi muziki wa ndani kwa kutoupa nafasi muziki wa mataifa mengine ndani ya nchi hiyo.

Kupitia nstastory yake kwenye mtandao wa Instagram Otile Brown amedai kuwa kwenye kiwanda cha muziki nchini Afrika Kusini kuna hali kujipa kipaumbele zaidi kwani nyimbo za wasanii wa ndani zinapiga sana kwenye maeneo ya umma tofauti na nchini ya Kenya ambayo imewazingatia sana wasanii wa nje huku akieleza kuwa inaweza kuwa moja kati ya sababu za muziki wao kuwa na thamani ya juu yenye maendeleo.

Otile Brown ambaye juzi kati amekuwa nchini Afrika Kusini amesema mfumo wa muziki wa Afrika kusini umewapelekea wasanii wengi kuwa na mafanikio makubwa hata wakiwa na kazi chache walizozifanya kwenye career yao ya muziki ambapo ameonekana kutoa changamoto kwa serikali ya kenya kufuata nyayo za nchi ya Afrika kusini ambayo imetengeneza mazingira ya kutumia sanaa kutoa ajira kwa maelfu ya vijana wake.

“Soko la muziki la Afrika Kusini halivumi sana lakini lina utajiri. Serikali imewatengenezea mazingirana wanajipenda sana unaweza kuwa na wimbo mkubwa Afrika na hawaujui maana huwezi sikia wimbo wa nje hata mmoja kwenye klabu, Migahawani au kwenye vyombo vya usafiri wowote”.

Otile anaendelea kwa kuandika “Ni ubinafsi ila imenifanya nifikirie Je ni bora uwe hivyo na watu wenu wawe vizuri au uwe muungwana waku support nyimbo za nje na kupoteza nguvu na thamani ya sanaa yenu maana jamaa kimya game wanailinda nakuithamini maana inatengeneza ajira 100% kila siku. Jamaa mtu ananyimbo mbili tu lakini mafanikio makubwa sana.” ameandika kupitia Instastory yake

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke