Mwanamuziki nyota nchini Otile Brown amelamba dili nono la kuwa balozi mpya wa Simu ya mkono ya Tecno Camon 19 kwa upande wa Kenya.
Otile Brown ametangaza habari njema kwa wafuasi wake kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kusema kwamba ana furaha kubwa kujiunga na familia ya Tecno inayojishughulisha na uzalishaji na usambazaji wa simu na vifaa vingine vya kielectroniki
“I am really thrilled and excited to officially announce my partnership with @tecnomobile @tecnokenya as their Brand Ambassador and the Chief Creative Officer for the TECNO CAMON 19 Series. Super Super Excited for this great partnership #CAMON19BA #TECNO #TECNOKENYA.” Otile Brown ameandika
Otile Brown sasa atatakiwa kutangaza bidhaa za Tecno kwa mashabiki zake kupitia mitandao ya kijamii kwa lengo la kuiongezea kampuni hiyo mauzo.