You are currently viewing OTILE BROWN AMTOLEA UVIVU WILLY PAUL KISA DISS-TRACK

OTILE BROWN AMTOLEA UVIVU WILLY PAUL KISA DISS-TRACK

Msanii Otile Brown ameonekana kumtupia dongo Willy Paul baada ya kudai kuwa anafanya kiki na matukio ili kuangaziwa.

Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram Otile Brown amesema hatua hii inasharia kuwa kuna wasaani ambao wameingiwa na wasiwasi kutokana na msukumo wakutaka kuzungumziwa huku akisema sio sawa.

Kauli ya Otile Brown inakuja mara baada ya Willy Paul kuachia diss-track iitwayo “Nikome” ambayo ilikuwa inamlenga mke wa msanii Bahati, Diana B, mchekeshaji Eric Omondi pamoja na wadau wengine kwenye tasnia ya muziki nchini.

Hata hivyo Willy Paul amefuta diss-track hiyo kwenye mtandao wa youtube mara baada ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kumshambulia.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke