You are currently viewing OTILE BROWN AMVUA NGUO MREMBO MWENYE SHAPE MATATA NCHINI KENYA VERA SIDIKA

OTILE BROWN AMVUA NGUO MREMBO MWENYE SHAPE MATATA NCHINI KENYA VERA SIDIKA

Staa wa muziki nchini Otile Brown amemtolea uvivu mrembo mwenye shape matata Vera Sidika baada ya mrembo huyo kuonekana kulitaja jina lake katika siku za hivi karibuni.

Kupitia instagram page yake Otile Brown amemtaka Vera Sidika kuitunza ndoa yake ikizingatiwa kuwa hajawahi kuizungumzia ndoa yake na mumewe brown mauzo sehemu yeyote kutokana na heshima aliyonao kwao.

“Jaribu kumheshimu mumeo na kulinda ndoa yako kama ninavyojaribu kunyamaza kila unapotaja jina langu. Dont get comfortable.” Ameandika kupitia insta story yake.

Kauli ya otile brown imekuja siku chache baada ya vera sidika kusema kuwa ikitokea otile brown anataka kufanya kolabo na mumwe Brown Mauzo ataunga mkono kikamilifu kolabo hiyo.

Hili halikutarajiwa kabisa kutoka kwa Vera Sidika ikizingatiwa kuwa alikuwa kwenye mahusiano na Otile Brown kipindi cha nyuma ambapo walikuja wakaachana vibaya baada ya kuingia kwenye ugomvi mbaya.

Kutokana na hilo inaonekana kwamba Vera sidika amepata furaha tena na labda alimsamehe Otile Brown ndiyo maana hajawahi kusema jambo lolote baya kumhusu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke