Staa wa muziki wa nchini Otile Brown amepokezwa tuzo ya Golden creators na mtandao wa youtube kwa kufikisha jumla ya subscribers millioni 1.
Mkali huyo wa “Jeraha” amewashukuru mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuendelea kufuatilia kazi zake ambazo zinaendelea kuonyesha mafanikio makubwa huku akiahidi kutoa mzuri kwa ajili yao .
Otile Brown anakuwa msanii wa kwanza kutokea Kenya kuwa na wafuasi wengi zaidi katika mtandao wa YouTube huku Dusuma aliyomshirikisha Meddy ikiwa ndiyo video yenye watazamaji wengi zaidi ikiwa na views milioni 35 ndani ya mwaka mmoja.
Baadhi ya wasanii kutoka Kenya wanaofuata kwa wafuasi wengi ni pamoja na Bahati Kenya akiwa na subscribers elfu 902K, Willy Paul 877K, Sauti Sol 856K, Khaligraph Jones 538K, na Nyashinski 473K.