Mkali wa muziki nchini Otile Brown amesifia uwezo wa msanii wa Bongofleva Harmonize katika verse ya wimbo wao wa pamoja waliofanya kwa mara ya kwanza.
Otile Brown ametumia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram kuelezea hilo, ambapo amesema Harmonize amefanya vizuri katika ngoma hiyo huku akieleza fahari yake kwa mashabiki wa Tanzania na Kenya ambao watakua tayari kusikia kazi hiyo.
Hivi karibuni Harmonize akiwa nchini katika ziara yake ya kimuziki alitangaza wazi kuja na ‘EP’ itakayo kuwa na nyimbo 5 za pamoja kati yake na Otile Brown.