Mwimbaji nyota wa kizazi kipya nchini Kenya, Otile Brown hataki kuwaacha mashabiki wake hivi hivi kabla mwezi huu haujaisha.
Hii ni baada ya kutangaza ujio wa ngoma yake mpya ambayo kwa mujibu wake itaingia sokoni Jumanne wiki ijayo, Januari 31.
Otile ameitaja ngoma hiyo aliyoipa jina la Shujaa wako kuwa ni kolabo yake ya Kimataifa akiwa na mwanamuziki kutoka nchini Tanzania, Ruby.
Hii itakuwa ni Kazi yake ya kwanza kwa mwaka 2023 ikizingatiwa kuwa hajaachia wimbo wowote tangu mwaka jana alipowabariki mashabiki zake na wimbo uitwao Do It alioshirikisha Vivian.