Staa wa muziki nchini Otile Brown, ametangaza kuachana na Mpenzi wake raia wa Ethiopia Nabayet baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa muda wa miaka mitatu.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Otile Brown amesema amechukua maamuzi ya kuachana na mpenzi wake huyo baada ya kuafikia makubaliano ya pamoja ambapo amedai kuwa wataendelea kuwa marafiki.
Hata hivyo chanzo cha wawili hao kuachana hajaweka wazi ila sio mara ya kwanza kufanya hivyo kwani kipindi cha nyuma wamekuwa na mazoea ya kuachana na kisha mwisho wa siku wanarudiana
Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wamehoji huenda Otile Brown anatengeza mazingira ya kumzinguziwa kabla ya ujio wa ngoma yake mpya
Ikumbukwe kuwa penzi la Otile Brown na Nabayet lilianza rasmi mwishoni mwa mwaka 2018 miezi kadhaa baada ya kuachana na aliyekua mpenzi wake Verah Sidika.