You are currently viewing Otile Brown awajibu waliomjia juu kuhusu Kiswahili

Otile Brown awajibu waliomjia juu kuhusu Kiswahili

Mwanamuziki nyota nchini Otile Brown ameamua kuwajibu wanaoendelea kumponda mtandaoni baada ya kutoa maoni yake kuwa lugha ya Kiswahili inayotumika na wasanii wa Kenya ndio sababu kubwa inayowafanya wasifanye vizuri kimataifa kama wanavyofanya wasaniii wa Nigeria.

Kupitia mfululizo wa instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Otile amesema kuwa lugha ya Kiswahili ndio lugha ambayo imempa mafanikio makubwa kisanaa huku akiwataka wanaomkosoa kuelewa kwanza alichokisema kabla ya kuleta ubishi.

Hitmaker huyo “I Need You” amesema hakuwa na nia ya kuishusha lugha ya Kiswahili ambayo imemtoa kimuziki ila alikuwa anajaribu kuanzisha mjadala utakaowasaidia wasanii wa Kenya kuchanganya lugha ya Kiingereza kwenye nyimbo ili waweze kupenya kimataifa.

Hata hivyo amemalizia kwa kusisitiza kuwa ataendelea kuimba nyimbo zake kwa lugha ya Kiswahili huku akitoa changamoto kwa jumuiya ya Afrika Mashariki kuendeleza mjadala wa lugha kwenye nyimbo za wasanii kama njia moja ya kupata suluhu ya kizingiti inayokwamisha muziki wa ukanda huu kufika kimataifa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke