You are currently viewing OTILE BROWN KUACHIA UPTOWN FLEX EP ALHAMISI HII

OTILE BROWN KUACHIA UPTOWN FLEX EP ALHAMISI HII

Msanii nyota nchini Otile Brown ametangaza kuachia EP mpya chini ya  lebo yake ya muziki ya Just in Love ambayo ni zawadi kwa mashabiki zake kuelekea siku ya wapendanao maarufu kama Valentines Day.

EP hiyo inakwenda kwa jina la Uptown Flex itakuwa na jumla ya nyimbo 5 ambazo amezifanya mwenyewe bila kumshirikisha msanii yeyote.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram Otile Brown ameshare artwork pamoja na Tracklist ya EP hiyo ambayo ina nyimbo kama  Double up, Realer, Fine By Me,  Run Up na Sempre.

Hata hivyo amewataka mashabiki zake kukaa mkao wa kula kuipokea Uptown Flex  EP ambayo itaingia sokoni rasmi Februari 10 mwaka wa 2022.

Hii inaenda kuwa EP ya kwanza kwa mtu mzima Otile Brown ikizingatiwa kuwa mwaka wa 202o aliwabariki mashabiki zake na Album iitwayo Just In Love ambayo ilikuwa na jumla ya mikwaju 11 ya moto.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke