Nyota wa muziki nchini Nigeria ambaye anaunda kundi la P-Square, Peter Okoye, ameweka wazi kuwa P-Square wana uwezo wakufanya matamasha bila kuachia kazi mpya na yakafanya vizuri.
Haya yanajiri baada ya wakali hao kuwakata mashabiki kuchagua kati ya ukumbi wa O2 Arena ama uwanja wa Wembley nchini Uingereza waende wakafanye show yao. Maoni ya mashabiki wengi yameuchagua ukumbi wa 02 Arena unaoingiza takribani watu elfu 20.
Chaguo hilo ni kutokana na hatua ya wasanii wa Nigeria kufanya show zao katika ukumbi huo na kutaka kuwashindanisha na wakongwe hao.
Wanamuziki tofauti tofauti wakubwa Kutoka Nigeria wamefanya matamasha yao katika ukumbi wa O2 na kuvunja rekodi ya mauzo ya ticketi zote/sold out, ikiwemo Wizkid , BurnaBoy na weekend iliyopita davido aliweza kuweka rekodi hiyo.
Ikumbukwe kuwa Kundi hilo lilivunjika miaka kadhaa iliyopita kabla ya kurudi hivi karibuni na kuanza kufanya shows mbalimbali kama awali.