Kundi la muziki la P-Square kutoka Nigeria ambalo kwa sasa limerejea tena, limetangaza ujio wa ziara yao ya kimuziki ya Dunia ‘World Tour’.
Kundi hilo linaloundwa na Peter na Paul Okoye, wametangaza hilo baada ya kukutana kwa mara ya kwanza jukwaani nchini Sierra Leone baada ya kumaliza tofauti zao zilizodumu kwa muda mrefu.
Kupitia video inayowaonesha wakitumbuiza kwenye tamasha la ‘Eco Fest’ huko Sierra Leone, wawili hao kwenye kurasa zao za instagram wameandika; “World Tour Loading……”
Hata hivyo, mapacha hao wanatarajiwa kutumbuiza pamoja Disemba 14 kwenye show yao ya kwanza waliyoipa jina la ‘P QSUARE REACTIVATED’.