Mwanamuziki Paa Kwaci ametangaza kuja na ziara yake ya nchini Marekani kuanzia mwezi Februari mwaka 2023.
Akizungumza na tovuti ya UrbanSpice msanii huyo mwenye makaazi nchini Canada amesema kwa sasa yupo kwenye matayarisho ya mwisho kukamilisha mipango ya tour yake hiyo.
Licha ya kutoanika mkeka wa miji ambayo ziara yake hiyo itapita, amesema aliamua kuja na wazo ya ziara hiyo kwa ajili ya kutanua wigo wa muziki ili iweze kuwafikia wengi.
Katika hatua nyingine, amedokeza ujio wa kolabo zake mbili ambazo amemshirikisha Rapa mkongwe Snoop Dog pamoja na Sean Kingston kwa kusema kuwa huenda ikaingia sokoni wiki ijayo, hivyo mashabiki wakae tayari kwa ajili ya kuupokea ujio wake mpya.