Mwanamuziki kutoka uganda Palasso amemtambulisha msanii wake mpya kwenye lebo yake ya muziki ya Team No Sleep.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema msanii wake anaitwa Carolina huku akimwagia sifa kwamba ana kipaji cha kipekee, hivyo ana Imani kuwa ataipeleka lebo yake kwenye ngazi ya kimataifa..
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Malamu” amesema Carolina atakuwa chini ya lebo ya team no sleep ambayo itasimamia kazi zake zote za muziki ambapo amewataka mashabiki zake wamkaribishe msanii huyo kwenye tasnia ya muziki nchini lakini pia wakae mkao wa kula kupokea nyimbo zake
“Karibu msanii kama wewe, mwenye kipaji, mrembo, Kijana na aliyejaa nguvu ni mali kwa kampuni kama yetu. Carolina sasa amesainiwa rasmi na Kampuni ya Team Good Music, Hongera. Hatuwezi kusubiri kuanza kufanya kazi na wewe. ,” Pallaso alitweet.
Kusainiwa kwa Carolina kunakuja miaka kadhaa baada ya msanii Jowy Landa kuigura lebo ya Team Good Music kwa njia tatanishi.
Utakumbuka mapema mwaka huu Palasso aliahidi kuwasaidia vijana wanaochipukia kwenye muziki nchini Uganda kwa kuanza kuwasaini ndani ya lebo yake ya muziki.