You are currently viewing PALASSO ATANGAZA KUJA NA ONESHO LAKE MWEZI JULAI MWAKA HUU

PALASSO ATANGAZA KUJA NA ONESHO LAKE MWEZI JULAI MWAKA HUU

Msanii nyota nchini Uganda pallaso ametangaza ujio wa   onesho lake la siku mbili litakalofanyika katika ukumbi wa Lugogo Cricket Oval.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Pallaso pamoja na uongozi wake wamesema onesho hilo litafanyika tarehe 1 na 2 mwezi julai mwaka wa 2022.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Malamu” ametoa rai kwa mashabiki zake kumuonyesha upendo na kumuunga mkono katika onesho lake hilo kwani hataki kutumbuiza kwenye ukumbi ambao hawana watu.

Cricket Oval ni ukumbi mkubwa maarufu uliopo jijini kampala wenye kuingiza idadi ya watu elfu 20 ambao unatumiwa na mastaa wakubwa duniani kufanya show zao.

Utakumbuka Pallaso kwa sasa anaendelea na Golden tour, ziara ya mwezi moja ambayo inalenga kuzunguka kwenye miji zaidi ya 25 nchini uganda ikitarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu wa Machi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke