Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Palasso anatarajia kuaza tour yake nchini humo ambayo itakuwa na show 25 kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Kupitia ukurasa wake rasmi wa instagram Palasso, ameipa ziara hiyo jina la Golden Tour na itaanza machi 6 hadi machi 31 mwaka wa 2022.
Ziara hiyo inatarajiwa kuzunguka kwenye miji mbalimbali nchini Uganda ikiwemo Lukaya, Katosi, Soroti, Kasanda na nyingine.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Maluma” amesema lengo la kuja na Golden tour ni kwa ajili ya kuwashukuru mashabiki zake ambao wamekuwa wakimsapoti tangu aanze safari ya muziki wake.