You are currently viewing PALLASO ADOKEZA MPANGO WA KUZINDUA KAMPUNI ITAKAYOSHUGHULIKA NA MATAMASHA YA MUZIKI

PALLASO ADOKEZA MPANGO WA KUZINDUA KAMPUNI ITAKAYOSHUGHULIKA NA MATAMASHA YA MUZIKI

Staa wa muziki nchini Uganda Pallaso amedokeza mpango wa kuja na kampuni itakayoshughulika na matamasha ya muziki.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Pallaso amesema amechukua hatua hiyo kama njia ya kuwaondoa madalali na mapromota ambao wamekuwa wakipora pesa nyingi kupitia kazi za muziki huku wakimlipa malipo duni.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Malamu” amesema kampuni hiyo pia itamsaidia kutanua wigo wa muziki wake uweze kuwafikia watu wengi duniani.

Pallaso ni moja kati wasanii ghali na waliopata shows nyingi nchini Uganda ambapo inadaiwa anatoza kati ya shillingi laki 3  na 6 za Kenya kwa shows za ndani ya nchi.

Utakumbuka Pallaso anajianda kuanza ziara yake ya kimuziki iitwayo Golden tour Machi 6 mwaka huu tour ambayo itazunguka zaidi ya miji 25 nchini kwa kipindi cha mwezi mmoja

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke