Mwanamuziki Pallaso Mayanja amekanusha madai ya kutengana na meneja wake, Kama Ivien.
Katika mahojiano, Pallaso amesema bado ana uhusiano mzuri wa kufanya kazi na Karma Ivien licha ya kutomtaja katika wimbo wake mpya “True Love”.
Pallaso amesema alizidiwa na mzuka akiwa studio, hivyo akasahau kumpa shavu meneja wake.
“Nitakapoacha kufanya naye kazi, nitaweka wazi kwenye kurasa zangu za mitandao ya kijamii. Bila tamko rasmi kutoka kwangu, usiamini uvumi huo,” Pallaso amebainisha.
Ikumbukwe mapema wiki iliyopita ripoti zilidai kuwa wawili hao waliingia kwenye ugomvi kutokana na masuala yanayofungamana na pesa.