You are currently viewing PALLASO AKASIRISHWA NA KITENDO CHA EDDY DEE KUMSEMA VIBAYA KWENYE VYOMBO VYA HABARI

PALLASO AKASIRISHWA NA KITENDO CHA EDDY DEE KUMSEMA VIBAYA KWENYE VYOMBO VYA HABARI

Staa wa muziki kutoka Pallaso Uganda hajafurahisha na kitendo cha prodyuza Eddy Dee kumuanika hadharani mbele ya mashabiki zake kuwa amekuwa akitumia studio yake kurekodi bila malipo.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Pallaso amesema ameshangazwa na hatua ya prodyuza huyo  kumzungumzia vibaya kwenye vyombo vya habari kuwa alidinda kumsaidia kumlipa kodi ya studio yake ikizingatiwa kuwa hakumpigia simu kumfahamisha masaibu anayoyapitia.

Prodyuza Eddy Dee ni rafiki yangu wa karibu na mshirika wa kibiasha ambaye ana mawasiliano yangu. Nashindwa mbona hakunitafuta. Hana ruksa kulipaka jina langu tope.

Kauli ya Pallaso imekuja mara baada ya kumpa prodyuza Eddy Dee shillingi milllioni moja za uganda alipe deni la kodi la shillingi millioni 4 anayodaiwa na mmiliki wa nyumba aliyopanga kwa ajili ya studio yake.

Utakumbuka juzi kati baada ya prodyuza huyo kufurushwa kwenye studio kutokana na deni la miezi saba ya kodi alijipeleka kwenye vyombo vya habari na kuwaanika wasanii waliokuwa wanatumia studio yake bila malipo akiwemo Pallaso.

Eddy Dee ameshatayarisha nyimbo za pallaso kama malamu what is money na nyingine nyingi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke