Msanii Pallaso alirejea kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda mwaka wa 2013 baada ya kuishi nchini Marekani kwa muda mrefu.
Pallaso ambaye alikuwa anajulikana kama Mr. Lizard alikaribishwa na marehemu Radio na Weasel kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda ambapo walirekodi wimbo wa pamoja uitwao Mudongo ambaye alifanya vizuri kwenye chati za muziki.
Pallaso alienda mbali zaidi na akafanya vizuri kama msanii wa kujitegemea ambapo alitunukiwa tuzo ya msanii bora wa mwaka kwenye tuzo za Zzina Awards.
Sasa akiwa kwenye moja ya Interview Pallaso amesema karibu amuombe kaka Weasel achukue nafasi ya marehemu Radio kwenye kundi la Goodlyfe crew lakini alikuja akaona kwamba itakuwa ni njia ya kumvunjia heshima mashabiki wa radio.
Ikumbukwe Pallaso alipata umaarufu kwenye tasnia muziki ya muziki nchini Uganda kipindi aliachia wimbo wake uitwao Malamu