Siku chache baada ya Ivan Karma kutishia kumfungulia mashtaka Pallaso kwa kuvunja mkataba wao wa miaka mitano ghafla, msanii huyo ameamua kutia neno juu ya tuhuma za meneja huyo wa muziki kutoka Uganda.
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni msanii huyo amesema hana muda wa kuzungumzia shtuma za ivan karma kwa kuwa anatumia jina lake kutafuta umaarufu mtandaoni.
Pallaso alisaini na uongozi wa Ivan Karma mwaka wa 2019 na tangu kipindi hicho ameachia nyimbo kali ambazo zimeacha alama kwenye tasnia ya muziki nchini uganda.