Msanii nyota kutoka Uganda Pallaso amelazimika kusitisha tamasha lake la muziki mara baada ya kuzidiwa na maumivu makali ya goti.
Pallaso ambaye juzi kati alifanyiwa upasuaji wa goti anasema anahitaji muda wa kutosha kuuguza majeraha aliyoyapata kwenye moja ya performance yake wiki kadhaa zilizopita kabla ya kurejea rasmi kwenye majukwaa ya muziki.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Mpa Love” amesema kwa sasa ameanza mazungumzo na uongozi wake kwa ajili ya kuja na tarehe nyingine ambayo ataanza kufanya tamasha lake la muziki ambalo lilipaswa kufanyika Juni 1 na 2 mwaka huu.
Hata hivyo Pallaso amesema hatoweza kuwapa mashabiki zake thamani ya pesa zao katika hali yake ya sasa ikizingatiwa kuwa amekuwa akitumbuiza kwenye shoo zake akiwa katika kiti cha magurudumu.