Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Pallaso amewachana mapromota wanaotilia shaka kiasi cha pesa anacholipisha kwa shows za ndani ya nchini.
Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Pallaso amewataka mapromota ambao wanasema hastahili kulipwa shillingi laki 2 za Kenya kwa show moja kutompa michongo ya shows zao kwani hana muda wa kuwashawishi kutokana ukubwa wa brand yake ya muziki.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Malamu” amejinasibu kwa kusema kwamba hakuna show hata moja ambayo imefanya vibaya tangu mapromota waanze kumpa shows huku akisisitiza kuwa anastahili kulipwa shillingi laki 2 kwa show moja kwani amewekeza pesa nyingi kujenga chapa yake kwenye kiwanda cha muziki nchini Uganda.