You are currently viewing PALLASO AWEKA WAZI KIASI CHA FEDHA ANACHOTOZA KWENYE SHOO ZAKE

PALLASO AWEKA WAZI KIASI CHA FEDHA ANACHOTOZA KWENYE SHOO ZAKE

Msanii nyota kutoka Uganda Pallaso ameamua kutaja kiasi cha pesa anacholipisha kwenye show zake iwapo utahitaji kufanya nae kazi

Katika mahojiano yake hivi karibuni Pallaso amesema analipisha kati ya shillingi millioni 15 hadi 20 za Uganda.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Malamu” amesema amechukua hatua hiyo kutokana na bidii anayoweka kila siku kwenye shughuli zake za muziki kwani amekuwa akiwekeza pesa nyingi kutoa muziki mzuri.

Utakumbuka Pallaso katika siku za hivi karibuni amekuwa akipokea shows nyingi kutoka kwa mapromota lakini pia ni  moja kati ya wasanii ghali nchini Uganda wanaolipwa mkwanja mrefu kwenye maonesho ya muziki kutokana na muziki wake kupendwa na wengi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke