Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Pallaso ameingia tena kwenye headlines mara baada ya kususia moja ya onesho lake huko Kyotera, masaka wikiendi hii iliyopita.
Duru za kuaminika znasema mashabiki walimsubiri pallaso kwa takriban masaa matatu lakini msanii huyo hakutokea kwenye performance yake, jambo lilowafanya mashabiki kuzua vurugu na kuaharibu kila kitu kwenye ukumbi wa burudani na kuacha mapromota wakikadiria hasara ya mamilioni ya pesa.
Juhudi za msanii Sheebah Karungi kuwatuliza mashabiki ziliambulia patupu kwani walionekana wenye hasira zaidi wakiwataka waliondaa onesho hilo kuwaregeshea pesa zao kwa kushindwa kutimiza ahadi ya kumleta pallaso jukwaani awape burudani.
Hii ni mara ya pili kwa pallaso kususia show, kwani mapema mwezi huu alijipata pabaya tena baada ya kushindwa kutokea kwenye moja ya show yake huko masaka, kitendo kilichowakera mapromota na mashabiki, na kama njia ya kuwaomba mashabiki zake msamaha alihamua kufagia mji wa masaka.
Utakumbuka Pallaso amekuwa akiendeleza ziara yake iitwayo Golden tour kwa kipindi cha mwezi mmoja ambapo amezunguka kwenye miji zaidi ya 25 nchini uganda kuw