You are currently viewing PALLASO: HUU NI MWAKA WANGU WA KUVUNA NILICHOKIPANDA KUPITIA MUZIKI WANGU

PALLASO: HUU NI MWAKA WANGU WA KUVUNA NILICHOKIPANDA KUPITIA MUZIKI WANGU

Nyota wa muziki nchini Uganda Pallaso ameibuka na kujigamba kuwa mwaka huu anaenda kuvuna pesa nyingi kupitia muziki ambao kwa mujibu wake ameufanyia uwekezaji mkubwa.

Akizungumza baada ya kutumbuiza kwenye private party moja viungani mwa jijini la Kampala Bosi huyo wa lebo ya Team Good music amesema kuwa huu ni mwaka wake  kuanza kuingiza kipato kupitia bidii yake kwenye kazi zake za muziki.

Hitmaker huyo wa “Nalonda Nemala” anasubiri kwa hamu kuanza kuingiza pesa atakapoanza kutumbuiza kwenye matamasha ya muziki pindi tu uchumi wa nchi ya Uganda itakapofunguliwa Januari 24 mwaka huu wa 2022 baada ya kufungwa kwa takriban miaka miwili kutokana na msala wa Korona.

Utakumbuka mwaka wa 2019 nyota ya pallaso ilianza kungaa kwenye muziki lakini kutokana na janga la korona hakuweza kuingiza pesa nyingi kupitia muziki wake baada ya matamasha kufungwa kama njia ya kuzuia msambao wa virusi vya corona.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke