Staa wa muziki kutoka nchini Uganda Pallaso ametusanua kuwa ataendelea na shows zake kama ilivyoratibiwa baada ya kupata jeraha la goti kwenye moja ya perfomance yake katika hoteli ya La Grande viungani mwa jiji la Kampala.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Malamu” ametumia mitandao yake ya kijamii kuwafahamisha mashabiki wake na wale waliokuwa wamempa shows hapo awali kwamba atumbuiza akiwa ameketi jukwaani hadi pale atakapopata nafuu licha ya kuumia goti.
“Niliumia goti kwenye jukwaa lililolegea katika Hoteli ya La Grande wakati nikitumbuiza jana usiku. Ilinibidi nifanye maonyesho yangu yote nikiwa nimekaa kwenye kiti, maumivu hayavumiliki lakini nitakuwa sawa. Nikiendelea kutafuta matibabu zaidi, nataka nifawahamishe kuwa shoo zote nilizopaswa kutumbuiza hazitaahirishwa. Lakini itabidi umnisamehe kwa kutumbuiza kwenye kiti hadi nitakapopata nafuu,” aliandika kwenye mitandao yake ya kijamii.
Ikumbukwe kwamba siku chache zilizopita, wadau pamoja na mashabiki wa muziki wake walimuashia moto kwa kususia baadhi ya shows zake licha ya mapromota kumlipa pesa zake zote.