You are currently viewing PAULA KAJALA AMUITA HARMONIZE BABA KWA MARA YA KWANZA

PAULA KAJALA AMUITA HARMONIZE BABA KWA MARA YA KWANZA

Hatimaye mtoto wa mpenzi wa mwanamuziki Harmonize, Kajala Masanja, aitwaye Paula kwa mara ya kwanza amemtambua Harmonize kama baba yake hadharani kupitia ukurasa wake wa instagram (insta story yake).

Paula amemtaja Harmonize kama baba yake akishare kionjo cha wimbo mpya wa Harmonize uitwao Amelowa.

Kupitia Instastory yake Paula amepost video hiyo na kisha kuandika “Baba unajua mpaka unajua tena”.

Paula hakuishia hapo ameenda mbali zaidi na kuandika, “Utaweza kukomoana na Jeshi wewe?”.

Utakumbuka wawili hao wamewahi kuwa katika tofauti kubwa kiasi cha Paula kutomtambua Harmonize kama baba yake alipomvisha mama yake Kajala Masanja pete ya uchumba, kitendo kilichopelekea walimwengu kuhisi kuwa bado ana kinyongo na baba yake Harmonize.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke