Kama ulikuwa unadhani penzi la Grand P na Eudoxie Yao limevunjika nikuambie tu pole. Mwanamuziki huyo mashuhuri kutoka Guinea amethibitisha kuwa bado anampenda mrembo huyo.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook Grand P ameposti mfululizo wa picha za kimahaba zaidi akiwa na Eudoxie ambapo amesisitiza kuwa ataishi kumpenda mwanadada huyo aliyebarikiwa na makalio makubwa kutoka Ivory Coast.
Hivi majuzi hata hivyo, Yao alidaiwa kuachana na bilionea huyo baada ya kumuona akijiburudisha na mwanadada mwingine kwenye moja ya night club.
Vyanzo vya karibu na wawili hao, vilisema mrembo huyo alihamua kubwaga manyanga baada ya kukithiri kwa tabia ya usaliti ambayo Grand P alikuwa nayo.