You are currently viewing PENZI LA HARMONIZE LAMPONZA KAJALA

PENZI LA HARMONIZE LAMPONZA KAJALA

Hakuna ubishi kuwa penzi la Staa wa Bongofleva toka Konde Music, Harmonize na Kajala linaendelea kutaradadi kila uchao baada ya wawili hao kurudiana wiki kadhaa zilizopita.

Kwa sasa Harmonize yupo katika ziara ya kimuziki jijini Goma, DR Congo na kwa kweli Kajala ameshindwa kuvumilia upweke nyumbani.

Muigizaji huyo ametumia ukurasa wake wa Instagram kuthibitisha mahaba yake kwa Harmonize na kumueleza jinsi anayompeza.

“I miss you @harmonize_tz💉😣❤,” Kajala aliandika kwenye Insta story yake.

Ujumbe huo ulijiri masaa machache tu baada ya Harmonize kutengeneza video kwa ajili ya mpenzi huyo wake.

Katika video hiyo Harmonize alionyesha upendo mkubwa kwa Kajala wakati anapokelea Dt Congo na kusema kuwa yuko pale ili kumfanya Kajala ajivunie.

“Nataka ujue kuwa niko hapa na nakupend sana. Najua uko mbali lakini sina la kufanya kwa sababu najua unajiandaa kwa siku yetu kubwa, najuvunia wewe na niko hapa kukufanya ujivunie,” alisema Harmonize.

Mwanamuziki huyo pia alitumia video hiyo kumshukuru mpenzi wake huyo kwa kumpa motisha ya kuchapa kazi yake ya muziki

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke