You are currently viewing PENZI LA HARMONIZE NA BRIANA LAINGIWA NA UKUNGU,HARMONIZE ATANGAZA KUWA SINGLE

PENZI LA HARMONIZE NA BRIANA LAINGIWA NA UKUNGU,HARMONIZE ATANGAZA KUWA SINGLE

Huenda penzi la mwanamuziki na C.E.O.wa KondeGang Harmonize na mpenzi wake mzungu raia wa Australia Briana limevunjika.

Kulingana na mfululizo wa post zake kupitia insta story yake kwenye mtandao wa instagram harmonize amesema kuwa haamini kama yupo singo tena.

Haikuishia hapo ameenda mbali na kuandika ujumbe ambao unahisiwakumlenga moja kwa moja mchumba wake Briana kwa kusema tuonane nikifikisha umri wa miaka 35 labda nina umri wa miaka.

Hata hivyo Harmonize hajatoa maelezo zaidi kuhusu kiini cha uhusiano wake na Briana kuvunjika  ila walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wamehoji kuwa huenda msanii huyo wa Bongofleva anatengeza  mazingira ya kumzungumziwa Afrika Mahariki kabla ya ujio wa ngoma yake mpya

Ikumbukwe kuwa penzi la Harmonize na Briana lilianza rasmi mwishoni mwa mwaka jana miezi kadhaa baada ya kuachana na aliyekua mpenzi wake Fridah Kajala.

Mbali na hayo mwanamuziki huyo ametangaza kuachia wimbo wake mpya siku ya kesho unaitwa ‘Mwaka Wangu’

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke