You are currently viewing PENZI LA MWANAMUZIKI GRAND P NA EUDOXIE YAO LAFUFUKA TENA

PENZI LA MWANAMUZIKI GRAND P NA EUDOXIE YAO LAFUFUKA TENA

Mwanamuziki mashuhuri kutoka Guinea Moussa Sandiana Kaba almaarufu Grand P amethibitisha kuwa bado anampenda soshalaiti Eudoxie Yao miezi kadhaa baada ya ripoti kuenea kuwa wametengana.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Grand P amesema ataishi kumpenda mwanadada huyo aliyebarikiwa na makalio makubwa kutoka Ivory Coast ambapo amedhihirisha upendo wake kwake usio na mwisho.

“Wewe na mimi ni wa maisha. Shukran” Grand P alimwandikia Yao.

Kauli ya Grand P imekuja siku chache baada Eudoxie Yao kumtaja bilionea huyo kama Ex wake baada ya kumuona akijiburudisha na wanadada wengine ndani ya bwawa la kuogelea.

Utakumbuka takriban miezi miwili iliyopita Grand P alidai kupokonywa mchumba wake Eudoxie Yao baada ya picha za mrembo huyo na mwanamuziki kutoka Congo Roga Roga kusambaa mitandaoni wakiwa wanajiburudisha, jambo ambalo lilimtia Grand P hofu kuwa huenda  Roga Roga alikuwa na nia ya kumpokonya mpenzi wake huyo.

Hata hivyo Grand P ambaye ana maumbile ya kipekee alimpa onyo kali Roga Roga dhidi ya kuendeleza mahusiano na mkewe.

“Ndugu yangu Roga Roga nakuheshimu sana wewe na watu wote wa Kongo… Lakini  njia unayotaka kufuata si ya kupendeza, usifurahie kuwa karibu na mke wangu la sivyo nitachukua hatua mbaya. Hii ni onyo, Asante!” Grand P aliandika kwenye mtandao wa Facebook.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke