You are currently viewing PENZI LA PRITTY VISHY LAMKOSESHA USINGIZI MADINI CLASSIC.

PENZI LA PRITTY VISHY LAMKOSESHA USINGIZI MADINI CLASSIC.

Msanii Madini Classic amethibitisha kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Ex wa Stivo Simple Boy Prity Vishy ikiwa ni miezi kadhaa wawili hao wamekuwa wakionekana pamoja.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Madini amesema alianza mahusiano yake kwenye mitandao ya kijamii alipomtumia ujumbe mfupi mrembo huyo na kumuomba namba ya simu huku akisema kwamba ujasiri na uhalisi wake ndio ilivutia sana.

“I met her on Instagram, I texted her and asked for her mobile number. We started there. I like her courage and she’s real,” Amesema Madini.

Hitmaker huyo wa ngoma ya Nilivyo amesema alipoweka wazi nia yake ya kutaka kumchumbia mrembo huyo, Vishy hakuamini na alisita kwa kuwa kipindi cha nyuma wasanii wengi wamekuwa wakimtafuta kwa ajili ya kufanya nae kazi.

Madini Classic amewataka walimwengu kutomshambulia Vishy kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa inamuumiza kwa sana.

“It really hurts me when I see people trolling her. She is an amazing personality when you get to interact with her and the trolls bring her energy down,” Amesema.

Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kutilia shaka madai ya Madini Classic na Pritty Vishy wakidai kuwa wana kazi ya pamoja wanafanya hivyo wanatumia suala hilo kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa mtandaoni.

“Ati babe…ata haiendani. Hii clout haijaenda shule bado.”  Shabiki mmoja ameandika kwenye Instagram.

 

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke