You are currently viewing PENZI LA RICK ROSS NA HAMISA MOBETO LINAZIDI KUKOLEA

PENZI LA RICK ROSS NA HAMISA MOBETO LINAZIDI KUKOLEA

Huba la mwanamitindo kutoka Tanzania Hamisa Mobeto na Rapa Rick Ross limekolea nazi.

Hii ni baada ya rapa kutoka Marekani, Rick Ross, Disemba 10 kumtakia heri ya kumbukumbu ya kuzaliwa Hamisa Mobetto ambaye alikuwa anasherehekea kutimiza miaka kadhaa tangu kuzaliwa kwake.

Rick Ross hajataka kuficha hisia zake kwa mrembo huyo na kumtamkia wazi akimuita ‘Baby’. “Happy birthday baby” – ameandika Rick Ross na Hamisa aliijibu komenti hiyo kwa madaha akiandika, “Thank you Daddy”.

Wawili hao wanahusishwa kuwa ni couple mara baada ya Novemba 25, mwaka huu kuonekana wakiwa katika falme za kiarabu Dubai wakila bata pamoja. Kubwa zaidi walionekana wakicheza muziki kwenye moja ya kumbi za starehe kwa kukumbatiana kimahaba

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke